WIZARA YA ELIMU YATOA MAFUNZO KWA VIONGOZI NA WATUMISHI KUHUSU MASUALA YA PROTOKALI

KATIKA  kuimarisha utendaji Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia inatoa mafunzo kwa viongozi na watumishi juu ya masuala ya Protokali kwa lengo la kuwajengea uwezo. Akifungua mafunzo hayo jijini Dodoma Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Francis Michael amewataka viongozi na watumishi hao kuhakiksha wanashiriki kikamilifu ili matokeo ya mafunzo hayo yaweze kuonekana katika utendaji.